| HENRY (KULIA) WAKATI AKIWA SIMBA |
Kiungo mkongwe wa Mtibwa,
Henry Joseph amefunguka kuwa hata yeye amekuwa haelewi kwanini Simba ilimuacha.
Henry ametua Mtibwa katika
usajili wa dirisha dogo msimu huu huku akiwa mwiba kwa Simba baada ya kuifunga
katika mchezo wa awali wa Kombe la Mapinduzi linaloendelea huko Zanzibar katika
ushindi ambao timu yake ya Mtibwa ilipata wa bao 1-0.
Henry alisema kuwa
anashukuru amekuwa katika kiwango kikubwa kwa sasa na amekuwa msaada kwa timu
yake ya Mtibwa lakini anashindwa kuelewa Simba ilifikiria nini wakati ule mpaka
ikafikiria kumuacha wakati bado msaada wake ulikuwa ukihitajika.
“Nashukuru nimeendelea
kudumu kwenye kiwango changu muda wote, nafikiri ni kujitambua tu ndiyo
kimesaidia ila huwa nashangaa sijui kwanini Simba iliamua kuniacha wakati ule,
sijajua walikuwa wanafikiria nini, ila hayo yamepita kwa sasa ninaangalia jinsi
ya kuisaidia timu yangu mpya,” alisema Henry kiungo wa zamani wa timu ya taifa,
Taifa Stars.







0 COMMENTS:
Post a Comment