January 4, 2015


COUTINHO AKISHANGILIA BAADA YA KUFUNGA BAO KWENYE UWANJA WA AMAAN, ZANZIBAR, LEO. 

Yanga sasa haikamatiki kwani ukiwasogelea, unakula zako nne.



Baada ya kuitwanga Taifa ya Jang'ombe kwa mabao 4-0 katika mechi ya Kombe la Mapinduzi, wamefanya hivyo tena kwa Polisi Zanzibar.

Katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar, Yanga ilipata mabao yake kupitia Andrey Coutinho aliyefunga mawili, Kpah Sherman na Simon Msuva.

Yanga ingeweza kufunga mabao mengi zaidi kutokana na kuutawala mchezo, lakini mara kadhaa wachezaji wake hawakutulia kwenye umaliziaji.

Wakati mwingine Polisi Zanzibar walilazimika kucheza kibabe ili kuwapunguza kasi wachezaji wa Yanga ambao walifunga mabao mawili kwa kila kipindi.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic