Watu
22 wamepoteza maisha katika vurugu za uwanjani nchini Misri na Shirikisho la
Soka la Misri limetangaza kuisimamisha ligi kuu nchini humo kwa muda
usiojulikana.
Watu
hao wamepoteza maisha baada ya kutokea vurugu kati ya polisi wa Misri dhidi ya
mashabiki wa zamalek.
Msemaji
wa Wizara ya Afya ya Misri, Hossam Abdel Ghafar, ametangaza watu watano
wameuwawa katika vurugu hizo zilizohusisha mechi kati ya Zamalek dhidi ya ENPPI.
Ghafar
amesema pamoja na watu hao watatu kuuwawa, wengine 34 wamejeruhiwa na wako
hospitali wanakopata matibabu.
Lakini
taarifa za vyombo vya habari zinaeleza, watu 22 wamepoteza maisha katika tukio
hilo.
0 COMMENTS:
Post a Comment