Kiungo nyota wa Rwanda ‘Amavubi’,
Jean Baptiste Mugiranezaa amefunga ndoa ya mpenzi wake wa siku nyingi, Gisa
Fausta.
Mugiraneza ndiye aliyefunga
bao wakati Taifa Stars Maboresho ilipotoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Amavubi
kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, hivi karibuni.
Kiungo huyo wa APR amekuwa
na bahati ya kuifunga Tanzania, kwani katika michuano ya Chalenji kwa nyakati
tofauti ameishafunga mabao mawili katika mechi mbili tofauti.
Mugiraneza sasa ameachana
na ukapera na sherehe za harusi yake zilihudhuriwa na wadau kadhaa wa michezo.
0 COMMENTS:
Post a Comment