Rais wa Rwanda, Paul Kagame
ambaye anajulikana kwa kupenda soka, ameonyesha wazi mapenzi yake kwa kikosi
cha Ivory Coast.
Kagame ameipongeza Ivory
Coast kutwaa ubingwa wa Afcon akiwa amefanya hivyo sambamba na bintiye, Ange.
Ange ametupia ujumbe kwenye
mtandao wa kijamaa wa Twitter kama ilivyo kwa baba yake yake akieleza
kufurahishwa na Tembo hao kutwaa ubingwa wa Afrika.
Ange ambaye pia ni
mwanajeshi licha ya kuwa mrembo hasa, ameeleza baada ya timu yake ya taifa ya
Amavubi, zaidi anasapoti Tembo hao wa Afrika Magharibi.
Ivory Coast chini ya
uongozi wa Yaya Toure imebeba ubingwa wa Afrika kwa kuishinda Ghana kwa mikwaju
9-8 ya penalti.
0 COMMENTS:
Post a Comment