Msemaji wa Mtibwa Sugar,
Thobias Kifaru amekiri kwamba mwenendo wa timu yake si mzuri.
Lakini akawashangaa
wanaoona amechanganyikiwa kutokana na Yanga kuifunga Mtibwa Sugar kwa mabao
2-0.
“Kweli utaona mambo si
mazuri sana kwetu, lakini hao wanaoona mimi nimechanganyikiwa pia hawana la
maana la kuzungumza.
“Mtibwa iliifunga Yanga bao
mbili, lakini ndiyo timu inayoonyesha soka safi hadi sasa. Sasa nachanganyikiwa
nini.
“Walio mkiani watafanyaje?
Mazoezi yanaendelea na kocha na wasaidizi wake wanafanya marekebisho, Mtibwa
itakaa vizuri tu, niamini? Alisema.
0 COMMENTS:
Post a Comment