Yanga, kesho Jumapili inatarajiwa
kushuka uwanjani kukipiga dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu Bara
kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, lakini kuna kitu cha kushangaza
kimetokea.
Beki wa kati wa Mtibwa Sugar, Salum Mbonde ameibuka
na kuipangia Yanga kikosi ambacho anaamini kinaweza kusaidia timu hiyo ya
Jangwani kupata ushindi kwenye mchezo huo.
Mbonde ambaye pia aliibuka Mchezaji Bora wa
Kombe la Mapinduzi 2015, amesema kuwa Yanga inatakiwa kutowachezesha Kpah
Sherman na Amissi Tambwe katika mchezo huo.
“Tunakutana na Yanga kwa mara nyingine tena
baada ya kuwafunga kwenye mechi ya kwanza, mimi nawapa ushauri tu kuwa, kama
wanataka ushindi katika mchezo wetu huo, basi wanatakiwa kutowapanga akina
Tambwe na Sherman, badala yake wawaanzishe Hussein Javu, Danny Mrwanda na
wazawa wengine, vinginevyo itakula kwao.
“Wazawa wanajua jinsi ya kucheza mechi ngumu,
hao Tambwe na Sherman siyo wachezaji wabaya lakini kutufunga sisi itakuwa ni
ngumu,” alisema Mbonde.
Mtibwa iliifunga Yanga mabao 2-0 katika mechi
ya kwanza ya msimu huu kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.







0 COMMENTS:
Post a Comment