Beki George Michael amefungiwa mechi tatu kutokana na kosa la kumkaba mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe.
Michael amekutwa na kosa baada ya gazeti maarufu la michezo la Championi kuchapisha picha akimkaba kwa juhudi kubwa mshambuliaji huyo wa Yanga.
Awali kamati ya nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lilitoa adhabu kwa beki Aggrey Morris wa Azam FC na Juma Nyosso wa Mbeya City waliokuwa na makosa.
Lakini likaamua kuweka kiporo suala la Michael kabla ya kutangaza leo.
Adhabu hiyo inahitimisha mzozo uliosababishwa na picha hiyo bora kabisa kuchapishwa katika gazeti kwa kipindi cha miaka kadhaa.
Picha hiyo ilizua gumzo kubwa katika anga za michezo nchini na huenda ikawa funzo kwa wachezaji watukutu na wakatili kwa wenzao.
0 COMMENTS:
Post a Comment