Kocha wa Real Madrid,
Carlo Ancelotti sasa atakuwa na amani moyoni kwa kuwa beki wake, Pepe amerejea.
Kwa mujibu wa
kitengo cha afya cha Real Madrid, Pepe sasa yuko poa na anaweza kucheza mechi
zinazofuata.
Pepe ambaye kuumia
kwake kulifanya safu ya ulinzi ya Real Madrid iyumbe kinoma, sasa amerejea.
Amekuwa akiaminika
kama kiongozi wa safu ya ulinzi ya Madrid akisaidiana na Sergio Ramos.
Jumatano, Madrid
itakuwa na kazi ngumu ya kuivaa Schalke 04 ya Ujerumani na watakuwa na nguvu
zaidi kutokana na kurejea kwa beki huyo kisiki.








0 COMMENTS:
Post a Comment