Timu ya
Taifa ya Tanzania ya Mpira wa Miguu wa Ufukweni (Beach Soccer) jana imeibuka na
ushindi wa mabao 5- 3 ugenini dhidi wa wenyeji timu ya Taifa ya Kenya kwenye
mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa fukwe za Hotel ya Big Tree Pirates jijini
Mombasa.
Katika
mchezo huo mabao ya Tanzania yalifungwa na Ali Rabbi mabao manne na
Mwalimu Akida bao moja .
Kipindi cha
kwanza kilimazika kwa Tanzania kupata mabao 2 Kenya 1, kipindi cha pili
kilimalizika Tanzania 4 Kenya 3 na kipindi cha tatu na cha mwishokwa mchezo
kimalizika kwa Tanzania kupata mabao 5 Kenya 3.
Mechi ya
marudiano inatarajiwa kuchezwa jumamosi wiki hii Februari 21, 2015 jijini Dar
es salaam, na endapo timu ya Taifa ya Tanzania itafanikiwa kuwatoa Kenya,
itacheza na timu ya Taifa ya Misri katika hatua inayofuata.
Mchezo wa
kwanza utafanyika kati ya tarehe 7,8 Machi 2015 jiji Dar es salaam na marudiano
yatafanyika nchini Misri kati ya tarehe 13,14 Machi 2015.
Timu
inarejea leo jijini Dar es salaam majira ya saa 11 jioni ikitokea jijini
Mombasa nchini Kenya.








0 COMMENTS:
Post a Comment