Yanga itapata uhakika leo kama itaweza kumtumia nahodha wa Yanga,
Nadir Haroub ‘Cannavaro’.
“Cannavaro hana uhakika mpaka sasa, aliumia goti kwenye mazoezi
lakini ameanza mazoezi ya peke yake jana (juzi), lakini huu siyo muda wa
kuzungumzia pengo lake, tunao wachezaji wengine wenye uwezo mkubwa,” alisema
Pluijm.
Hata hivyo imeelezwa kwamba tayari timu ya tiba ya Yanga ikiongozwa
na Dk Juma Sufiani imeanza kushughulikia suala hilo.
Cannavaro ni mhimili wa ulinzi katika kikosi cha Yanga licha ya
kwamba ina wachezaji wengi wanaoweza kuziba nafasi hiyo.








0 COMMENTS:
Post a Comment