February 25, 2015


Kocha wa Mwadui FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ametua katika kikosi cha Coastal Union na kuanza kazi.


Julio anatua Coastal kama sehemu ya ‘urafiki’ wake na klabu hiyo ili kusaidia kuboresha benchi la ufundi.


Tayari Coastal Union iko chini ya Kocha Mkenya, James Nandwa lakini mwendo wake umeonekana kutowaridhisha Wanatanga.

Julio alitua kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga na kuzungumza na wachezaji.
Kabla ya hapo alifanya mazungumzo na viongozi wa Coastal Union.

Viongozi aliozungumza nao ni pamoja Kocha Mkuu, James Nandwa, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Coastal Union, Albert Peter, Katibu Mkuu Coastal Union, Kassim El Siagi na Meneja wa Coastal Union, Akida Machai.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic