Na Louis Ngwako, Gaborone
YANGA wanashuka dimbani leo kwenye Uwanja wa Lobatse ulio kilomita
70 kutoka katika Jiji la Gaborone kucheza mechi ya pili ya Kombe la Shirikisho
dhidi ya BDF XI.
Ukiwa na idadi ya wakazi wapatao 30,000 tu, Mji wa Lobatse upo
Kusini Mashariki mwa Gaborone na Uwanja wa Lobatse wenye uwezo wa kuingiza watu
20,000 walioketi uko katikati ya mji huo.
Ukizungumzia kwa ukubwa, Lobatse unashika nafasi ya tatu baada ya
Francistown ulio katika Mji wa Francis, unaoingiza watu 27,000.
Francistown ndiyo uwanja mkubwa zaidi nchini hapa na unafuatiwa na
Uwanja wa Taifa wa Gaborone unaoingiza watu 22,500. Halafu Lobatse.
Nyuma ya Uwanja wa Lobatse, Mto Peleng unakatiza na hali ya hewa ya
eneo hilo ni baridi mara nyingi kwa kuwa unazungukwa na milima.
Una vyumba vinne vya kubadilishia nguo, viwili vya wanaume na viwili
vya wanawake, chumba kimoja cha wauguzi, waamuzi, pia mageti makubwa matano ya
kuingilia uwanjani.
Kuna marekebisho makubwa yanaendelea kwa ajili ya kuuboresha,
yanatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.
Usisahau, uwanja unaomilikiwa na BDF XI unajulikana kama SSKB, upo
hapa jijini Gaborone na unaingiza watu 5,000 walioketi na unashika nafasi ya 11
kwa ukubwa wa viwanja nchini hapa.
UWANJA UWEZO MJI
1. Francistown 27,000
Francistown
2. Taifa
22,500
Gaborone
3. Lobatse 20,000
Lobatse
4. Molepolole 15,000 Molepolole
5. Maun 10,000 Maun
SOURCE: CHAMPIONI
0 COMMENTS:
Post a Comment