February 28, 2015



Kipindi cha pili, Simba imefanikiwa kufunga mabao mawili kupitia Emmanuel Okwi na Ramadhani Singano ‘Messi’.


Simba ingeweza kufunga zaidi ya mabao matatu lakini walipotea nafasi nyingi za kufunga.



Huu ndiyo ushindi mkubwa zaidi kwa Simba msimu huu.
MAPUMZIKO:

Dk 44, Singano anakosa bao baada ya mpira wake kupita kidogo juu ya lango la Prisons kipa akiwa ametoka.

GOOOOOOOO Dk 42 Ajib anafunga bao la tatu kwa mkwaju wa penalti baada ya beki kunawa eneo la 18.

Dk 38, Simba wanafanya shambulizi jingine kali, lakini licha ya Sserunkuma kutoa pasi safi, Ajib, Ndemla na Singano wanashindwa kuitumia.
Dk 34 Prisons wanamuingiza John Matei kuimarisha safu ya kiungo.
 
Dk 30, Sserunkuma anafunga baada ya kuuwahi mpira baada ya kipa kuutema, lakini mwamuzi anasema alimgonga kipa.


Dk 29, Mkude anaingia vizuri lakini pasi yake ya nguvu inamshinda Ajib ambaye anautoa nje na kuwa goal kick.

Dk 24, Simba wanapata kona baada ya kipa Prisons kuokoa mpira wa adhabu wa Ajib.


GOOOOOOOOOO DK 21, Ajib tena anaifungia Simba bao la pili baada ya kipa Prisons kutema mpira na yeye kumpiga chenga na kuutupia wavuni.


Dk 18, Ajibu tena anaingia katika eneo la hatari lakini mabeki wa Prisons wanaokoa na kuwa kona
GOOOOOOOOO Dk 16, Ajibu anaifungia Simba bao kwa shuti kali baada ya pasi murua ya Sserunkuma aliyewachanganya mabeki wa Prisons.

Dk 13, Sserunkuma anaruka kupiga kichwa krosi nzuri ya Jonas Mkude, lakini unatoka nje.
Dk 11, krosi nzuri ya Messi inamfikia Ajib lakini anashidnwa kufunga baada ya mabeki wa Prisons kuuzuia mpira.

DK 4, Sserunkuma anajaribu kuuwahi mpira wa faulo uliotemwa na kipa lakini anachelewa


Mpira unaanza kuchezwa zaidi katikati ya uwanja kutokana na timu zote kuonekana kama zinasomana.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic