February 12, 2015


Yanga itamkosa mshambuliaji wake Danny Mrwanda katika mechi dhidi ya BDF XI ya Botswana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, keshokutwa.


Mrwanda analazimika kuwa karibu na mkewe ambaye amejifungua mtoto wa kike kwa kufanyiwa upasuaji.

Kocha wa Yanga, Hans van der Pluijm ameiambia SALEHJEMBE, tayari ametuma salama za pongezi kwa Mrwanda.

"Tayari nimetuma salamu, tunamtakia kila la kheri na mkewe apone haraka.

"Tumempa ruhusa kwa kuwa anahitajika kuwa karibu na familia yake na sisi tutapambana kwa upande wetu," alisema Pluijm.

Waswana hao wanatarajia kutua jijini Dar, usiku huu tayari kuivaa Yanga hiyo Jumamosi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic