Klabu
ya Red Arrow FC inayoshiriki Ligi Kuu nchini Zambia inatarajiwa kuwasili jijini
Dar es salaam-Tanzania jumatatu ya wiki ijayo kwa ajili ya kuweka kambi ya
mafunzo ya wiki moja kujindaa na msimu mpya wa Ligi Kuu nchini humo 2015.
Uongozi
wa klabu hiyo chini ya mwenyekiti wake Col Nolacso K Chilando ulifika leo makao
makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania - TFF sambamba na Afisa
habari wa klabu Lt Col Melody Siisii, Bw Alex Chila ofisa ubalozi wa Zambia
nchini Tanzania kujitambulisha uwepo wao nchini.
Wakiongea
na katibu mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania - TFF
Selestine Mweisgwa, uongozi wa timu hiyo umesema maandalizi ya kambi
yameshakamilika na kikubwa walikua wanaliomba Shirikisho la Mpira wa Miguu
nchini kutambua uwepo wao na kuwasaidia kupata viwanja vya kufanyia mazoezi.
Naye
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini -TFF Bw.Mwesigwa
alisema wameyapokea maombi hayo ya Red Arrow FC na kuwakaribisha nchini
kwa ajili ya kambi yao na kusema ujio wao utafungua milango kwa vilabu vingine
pia kuja kuweka kambi nchini.
Timu
ya Red Arrow FC inayomilikiwa na jeshi la Anga nchini Zambia ikiwa nchini kwa
mafunzo, inatarajia kucheza mchezo mmoja wa kirafiki na imeliomba Shirikisho la
Mpira wa Miguu nchini kuwatafutia timu moja ya kucheza nayo.
0 COMMENTS:
Post a Comment