| KASEJA (KATIKATI) AKIWA MAHAKAMANI PAMOJA NA MWANASHERIA WAKE (KUSHOTO) NA MWANASHERIA WA YANGA, CHACHA. |
Kesi inayomkabili aliyekuwa kipa wa Yanga, Juma Kaseja leo ilitakiwa kuanza kusikilizwa sasa imeahirishwa hadi Machi 10, mwaka huu.
Kesi hiyo ilipangwa
kusikilizhwa katika Mahakama ya Kazi kitengo cha upatanishi lakini imeahirishwa
na Hakimu Fimbo kufuatia ofisi ya Mawakili inayomuwakilisha Kaseja, Mbamba Advocates
kukumbwa na janga la kuungua moto
na hivyo kupoteza nyaraka muhimu zikiwemo zilizokuwa zikihusu kesi hiyo.
Wakili aliyemuwakilisha
Kaseja mahakamani hapo ni Nestor Mwenda kutoka Mbamba Advocate. Upande wa Yanga
uliwakilishwa na Mkurugenzi wa Sheria wa timu hiyo, Frank Chacha.
Yanga inamdai Kaseja zaidi ya
Sh milioni 200 kwa madai alikiuka mkataba.
Hata hivyo, Kaseja ndiye
alikuwa wa kwanza kulalamika Yanga kuvunja mkataba kutokana na kushindwa
kumlipa kwa wakati mwafaka.
Baadaye Yanga ilimlipa nay
eye akaandika barua akitaka kurejea kazini lakini hakukuwa na majibu. Baada ya
kuona ukimya huo, Kaseja aliamua kwenda katika mazoezi ya Yanga kuungana na
wenzake, lakini akazuiwa na aliyekuwa Kocha wa Yanga, Marcio Maximo aliyesema
lazima apate maelekezo kutoka kwa uongozi.







0 COMMENTS:
Post a Comment