Kocha Mkuu
wa Prisons, David Mwamwaja amesema ana uhakika Yanga watahadithia kuhusiana
uwezo wa Prisons watakaporejea jijini Dar.
Yanga
wako mkoani Mbeya kwa ajili ya mechi ya Ligi Kuu Bara itakayopigwa keshokutwa
kwenye Uwanja wa Sokoine.
Mwamwaja
amesema wana uwezo mkubwa wa kushinda mechi dhidi ya Yanga hata kama itakuwa
ngumu.
“Kweli
tunawaheshimu Yanga kama timu kongwe, lakini wanajua uwezo wetu na wanatambua
ugumu watakapokutana na sisi.
“Safari
hii tunataka kushinda na kubakiza pointi tatu Mbeya. Nakuambia wakirudi Dar
watawaeleza kazi ilivyokuwa.
“Tumejiandaa
vilivyo na tunajua namna pointi tatu zilivyo muhimu kwetu. Hatuwezi kufanya
utani,” alijigamba Mwamwaja ambaye kikosi chake kimekuwa na mwendo wa kusua,
hali iliyosababisha mashabiki kuanza kupiga kelele wakitaka afukuzwe.







0 COMMENTS:
Post a Comment