February 8, 2015


Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm amewaambia wachezaji wake, dawa ya kuondokana na kupoteza nafasi nyingi ni kuwa watulivu na kuachana na presha ya mashabiki kwa muda.


Pluijm raia wa Uholanzi, ameendelea kulizwa na wachezaji wake kupoteza nafasi za kufunga na kusema wanaweza kuzitumia vema kama wakijiondoa katika presha.

"Wachezaji wanachanganyikiwa kwa kuwa presha ni kubwa sana, wako wanataka kufunga kila mpira lakini wako ambao wanapata nafasi, lakini hawana utulivu.

"Yanga ni timu kubwa, presha ya mashabiki ipo juu na hii inawaathiri wachezaji.

"Nimezungumza nao mara kadhaa, nimesisitiza suala la presha na kuwaambia mashabiki wana haki yao katika kudai ushindi na mabao lakini wao wanapaswa kufanya kazi yao kwa ufasaha kwa mujibu wa tulichojifunza," alisema.

Yanga inashuka leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, kucheza mechi yake ya kwanza ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic