February 8, 2015


Kocha Mkuu wa Simba, Goran Kopunovic amesema kuna kila sababu ya mashabiki wa Simba kuendelea kumvumilia.


Amesema ana imani na kikosi chake kitakuwa na mabadiliko baada ya muda, lakini uvumilivu ndiyo dawa.
“Tumekuwa na vipindi vya kupanda na kushuka, utaona mechi moja tuko bora zaidi na nyingine tunashuka.

“Uvumilivu ndiyo jambo muhimu zaidi. Hatuwezi kufanikiwa kama leo tutachanganyikiwa na kuanza kufanya vitu nje ya msitari.

“Sare na Coastal si tulichokitaka, lakini angalau hatujapoteza mchezo tunaweza kuendelea kujipanga,” alisema Kopunovic raia wa Simba.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic