Klabu
ya Chelsea imetangaza kuingia mkataba na kampuni ya kuuza matairi ya magari ya Yokohama
ya nchini Japan.
Kwa
hapa nyumbani, kampuni ya Bin Slum Tyres ndiyo imekuwa iking’ara katika klabu
za Ligi Kuu Bara ikiwadhamini Mbeya City, Stand United na Ndanda FC.
Msimu
ujao, Chelsea itaanza kujimwaga Yokohama na kuachana na Samsung ambayo wamekuwa
wakiitumia na mkataba wao unaisha mwishoni mwa msimu huu.
Yokohama
itakuwa ikimwaga pauni milioni 40 kwa mwaka katika klabu hiyo inayomilikiwa na Mrusi,
Roman Abramovich.
Mkataba
wa Chelsea na Yokohama utakuwa wa miaka mitano na wa pili kwa ukubwa ukifuatiwa
ule wa Manchester United na kampuni ya magari ya Chevrolot ambayo inamwaga
pauni milioni 53 kwa mwaka.
0 COMMENTS:
Post a Comment