February 26, 2015


Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amepeleka salamu za rambirambi kwa familia ya  Mohamed Nyama, kufuatia kifo cha mwamuzi mstaafu Mohamed Nyama ambaye pia aliwahi kuwa mjumbe wa kamati ya waamuzi  ya TFF kilichotokea jana kwao Nachingwea- Lindi.


Marehemu Nyama wakati wa uhai wake alikuwa mwamuzi wa daraja la kwanza ambaye pia alitambuliwa na FIFA, Nyama anatarajiwa kuzikwa leo jioni kwao Nachingwea mkoani Lindi na TFF 
itawakilishwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Athumani Kambi.


Katika salam zake kwa familia ya Nyama, kwa niaba ya TFF, familia ya mpira wa miguu na watanzania Rais Malinzi amewapa pole wapenzi wa mpira wa miguu nchini  katika kipindi hiki kigumu cha maombelezo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic