Shirikisho
la Mpira Soka Tanzania (TFF), limezitakia kila la kheri na ushindi
timu za Azam na Young Africans katika michezo yao ya marudiano itakayofanyika
mwishoni mwa wiki hii .
Azam
FC itakuwa ugenini siku ya jumamosi mjini Khartoum, Sudan kucheza mchezo wa
marudiano na wenyeji timu ya El Merreikh ambapo katika mchezo wa awali
uliofanyika Chamazi jijini Dar es salaam Azam iliibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Jijini
Gaborone nchini Botswana katika kombe la Shirikisho, timu ya Young Africans
watacheza na wenyeji timu ya jeshi ya BDF XI siku ya ijumaa katika mchezo wa
marudiano pia, ambapo katika mechi ya awali Young Africans iliibuka na ushindi
wa mabao 2-0.
Mjini
Zanzibar KMKM wataikaribisha timu ya AL Hilal ya Sudan siku ya jumamosi katika
Uwanja wa Aman, huku kikosi hicho Maalum cha Kuzuia Magendo kikihitaji ushindi
wa kuanzia mabao 3-0 ili kuweza kusonga mbele, kufuatia kupoteza mchezo wa
kwanza Khartoum kwa mabao 2-0.
Timu
ya Polisi Zanzibar itakuwa mwenyeji wa timu ya FC Mounana kutoka nchini Gabon
siku ya Jumapili katika mchezo wa kombe la shirikisho barani Afrika,ikihitaji
ushindi wa mabao 5-0 ili kufuzu hatua inayofuata baada ya kupoteza mchezo wa
awali kwa mabao 4-0.
Kwa
niaba ya TFF, famili ya mpira na watanzania
wote wanawatakia kila la kheri na ushindi katika michezo hiyo ya marudiano
ambapo timu hizo zitakua zikipeperusha bendera ya Taifa.
0 COMMENTS:
Post a Comment