| KOCHA WA TOTO, JOHN TEGETE AKIWA NA WACHEZAJI WA TOTO. |
Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania
(TPLB) imethibitisha ushindi wa pointi na mabao matatu kwa timu za Majimaji na
Toto Africans baada ya mechi zao za Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kuvurugika
kutokana na sababu mbalimbali.
Toto Africans imepewa ushindi huo kwa mujibu wa Kanuni ya 41(3) ya
FDL baada ya vurugu za washabiki wa Geita Gold kusababisha mechi hiyo
iliyochezwa Februari 10 mwaka huu kwenye Uwanja wa Nyankumbu mkoani Geita
kuvunjika dakika ya 12.
Pia Kamati hiyo iliyokutana Dar es Salaam jana (Februari 12 mwaka
huu) imezuia mechi za FDL kuchezwa kwenye uwanja huo ambao hauna uzio wa
kutenganisha wachezaji na washabiki kwa sababu za kiusalama.
Friends Rangers imepoteza mechi hiyo kwa mujibu wa Kanuni ya 28(1)
ya FDL, Majimaji kama ilivyo Toto Africans imepewa ushindi wa pointi tatu na
mabao matatu.







0 COMMENTS:
Post a Comment