Mchezaji Venance Joseph wa Geita Gold ambaye alimpiga kichwa refa
akipinga adhabu ya penalti iliyotolewa dhidi ya timu yake kwenye mechi hiyo
amesimamishwa wakati akisubiri kosa lake kusikilizwa na Kamati ya Nidhamu ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Malalamiko ya Friends Rangers kwenye mechi dhidi ya Majimaji
yametupwa na kupigwa faini ya sh. 500,000 kwa kusababisha mchezo huo uliochezwa
Januari 29 mwaka huu Uwanja wa Majimaji mjini Songea kuvunjika dakika ya 39.
Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 28(4) ya FDL.
Naye Kocha wa Friends
Rangers, Herry Chibakasa (Mzozo) suala lake limepelekwa kwenye Kamati ya
Nidhamu ya TFF ili aweze kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa mujibu wa Kanuni ya
39(8) ya FDL kwa kuhamamisha vurugu kwenye mechi dhidi ya Majimaji.
Mwamuzi John Mafuru wa Mbeya aliyechezesha mechi ya Majimaji na
Friends Rangers amefungiwa miezi 12 (kumi na mbili) kwa kutozingatia sheria
kiasi cha kuvuruga mchezo. Adhabu hiyo imezingatia Kanuni ya 37(1) ya FDL.








0 COMMENTS:
Post a Comment