March 16, 2015


Beki mahiri na mkongwe wa Mbeya City, Juma Nyosso, amebakiza mechi mbili kabla ya kurejea tena dimbani.


Nyosso amekaribia kabisa kumaliza adhabu yake ya kufungiwa mechi nane na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF). Alifungiwa kutokana na gazeti hili kutoa picha inayoonyesha akimdhalilisha straika wa Simba, Elias Maguli katika mchezo baina ya timu hizo, Januari 28, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

Mpaka sasa, beki huyo amekosa michezo sita ambayo ni dhidi ya Yanga, Mtibwa Sugar, Ruvu Shooting, JKT Ruvu, Coastal Union na Mgambo JKT.

Wakati wote akiwa nje, timu yake iliambulia sare nyingi na kabla ya mechi ya jana dhidi ya Mgambo, ilikuwa nafasi ya pili kutoka mkiani ikiwa na pointi 19, zikimaanisha kwamba ina hatari ya kuwa miongoni mwa timu mbili zitakazoshuka daraja msimu huu.


Mechi nyingine mbili ambazo Nyosso atazikosa ni dhidi ya Stand United na ya mwisho dhidi ya Azam FC, kisha rasmi atarejea uwanjani kuivaa Ndanda kwenye Uwanja na Nangwanda Sijaona Aprili 4, mwaka huu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic