March 7, 2015


Chama cha Soka cha England (FA), kimemfungia kucheza mechi saba straika wa Newcastle United, Papiss Cisse kutokana na kukiri kumtemea mate beki wa Manchester United, Jonny Evans.
Evans ameendelea kukomaa kwamba hakumtemea mate Msenegali huyo ingawa picha zinaonyesha naye alifanya hivyo. Suala lake litasikilizwa leo.

TFF pia ilimfungia beki Juma Said 'Nyosso' baada ya gazeti la Michezo la Championi kupiga picha akimdhalilisha Elius Maguri wa Simba. FA yenye inatumia picha ya gazeti la Daily Mail lililonasa kitendo hicho.

Cisse na Evans waliingia katika mzozo kipindi cha kwanza wakati timu zao zilipokutana kwenye mchezo wa ligi kuu Jumatano iliyopita ambapo Man United ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

Cisse tayari amekubali kutumikia adhabu hiyo iliyotolewa na FA huku Evans naye akitarajiwa kufungiwa mechi sita kama atapatikana na hatia ya kurudishia kumtemea mate mwenzake kutokana na taarifa ya ripoti ya mchezo huo uliochezeshwa na Anthony Taylor kutoonyesha tukio hilo na kulazimisha chama hicho sasa kutumia picha za video.



Alhamisi iliyopita, Cisse alikubali kutenda kosa hilo ambalo adhabu yake mara zote imekuwa ni kufungiwa mechi sita, lakini FA ikaamua kumfungia saba kutokana na sheria ya kifungu cha E1 [a] kinavyosema.

Evans wakati akitoa maelezo yake alidai alishangazwa kuona Cisse akimtemea mate lakini baada ya kitendo hicho alijaribu kumuomba msamaha, jambo lililompandisha hasira beki huyo.

Msimu huu, FA ilikubali kuangalia kuongeza adhabu kwa kosa la kutemeana mate ndani ya uwanja ili kuhakikisha kosa hilo linaondoka kwenye mchezo wa soka japokuwa sheria za Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) ni kufungiwa michezo sita.


Cisse amepewa adhabu hiyo kutokana na Desemba, mwaka jana, kutolewa kwenye mchezo dhidi ya Everton baada ya kumfanyia vurugu nyota wa timu hiyo, Seamus Coleman.

Katika vurugu hizo alizofanya dhidi ya Coleman, Cisse alijikuta akifungiwa kucheza michezo mitatu ya ligi na ndiyo sababu kubwa iliyoifanya FA kumuongezea adhabu yake.

Evans kama atapatikana na hatia juu ya utata huo, inamaanisha kuwa atazikosa mechi za Premier League dhidi ya Spurs, Liverpool, Manchester City na Chelsea, ambapo jana jioni FA ilitarajia kutoa msimamo wake juu ya beki huyo.

Newcastle yalaani
Uongozi wa klabu hiyo kupitia kwa mkurugenzi wake mtendaji, Lee Charnley, ulisema: “Wote wanastahili adhabu lakini kwa Papiss kukiri alifanya kitendo hicho ni tabia ambayo inaonyesha alistahili kuvumiliwa.”
Hata hivyo, Cisse ambaye ni mfungaji anayeongoza katika kikosi cha Newcastle kwa mabao yake 11, timu yake imeamua kumkata mshahara wake wa wiki moja ambao ni pauni 40,000 (Sh milioni 108), kutokana na kosa hilo.

Mechi za Premier atakazozikosa
Everton (ugenini), Machi 15
Arsenal (nyumbani), Machi 21
Sunderland (ugenini), Aprili 5
Liverpool (ugenini), Aprili 13
Tottenham (nyumbani), Aprili 19
Swansea (nyumbani), Aprili 25

Leicester (ugenini), Mei 2

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic