KAGERA SUGAR |
Kagera Sugar imeikomalia Coastal Union
nyumbani kwao Mkwakwani mjini Tanga kwa sare ya mabao 2-2.
Mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara ilikuwa ngumu na
kipindi cha pili kilionekana kuwa kigumu kwa Coastal Union ambayo ilitawala
kipindi cha kwanza.
Mabao mawili ya Coastal yalifungwa na Mkenya
Rama Salim kwa penalti na Selemani Kibuta katika dakika ya 7 mapema kabisa.
Lakini Kagera wakasawazisha kupitia Atupele
Green katika dakika ya 52 na Rashid Mandawa akapiga la pili dakika ya 87.
0 COMMENTS:
Post a Comment