NANDWA AKIWA NA WACHEZAJI WAKE WA COASTAL UNION SIKU CHACHE KABLA YA KUTANGAZA KUJIUZULU. |
Uongozi wa timu ya Coastal Union ya Tanga,
umefunguka na kutaja sababu zilizopelekea kocha wao, James Nandwa, kukabidhi
barua ya kuacha kazi juzi Jumatatu jioni kwa kile walichosema kuwa hakutimiza
malengo yake.
Tayari, Coastal wamemkabidhi kikosi Jamhuri
Kihwelo ‘Julio’ ambaye atasaidiana na Joseph Lazaro ambaye alikuwa kocha wa
African Sports iliyopanda ligi kuu msimu huu.
Msemaji wa Coastal, Oscar Assenga, amesema
kuwa katika barua hiyo, Nandwa ambaye ni raia wa Kenya, alibainisha kuwa aliamua
kujiweka pembeni kutokana na timu kuendelea kufanya vibaya, tofauti na malengo
yake aliyojiwekea wakati anakuja.
“Katika barua yake, yeye alisema kuwa
hakuridhishwa na kiwango cha timu na hakujua sababu za kuendelea kufanya vibaya.
Ameshinda mechi moja katika mechi saba, jambo ambalo yeye amesema kuwa si
kiwango chake kiufundishaji,” alisema Assenga.
Coastal mpaka sasa ndiyo imebadilisha makocha
mara mbili ndani ya msimu huu, ambapo ilianza ligi ikiwa na Mkenya, Yusuf
Chippo ambaye alitimkia FC Leopard ya nchini kwao.
0 COMMENTS:
Post a Comment