Nyota wa zamani wa Arsenal,
Thierry Henry aliwapa bonge la ‘surprise’ wanafunzi wa shule moja nchinI Wales.
Henry ambaye alikuwa hatari
kwa kucheka na nyavu, alizuga kama mwalimu na kuingia hadi darasani na kumpa
tuzo ya Pen-Y-Dre mwanafunzi Emma
Morgan.
Kwa sasa Henry ni
mtangazaji katika kituo cha runinga cha Sky Sports News, lakini alipoingia
wanafunzi walidhani ni mwalimu mpya ambaye moja alikwenda katika ubao na kuanza
kutoa somo.
Ilikuwa vigumu kwa
wanafunzi hao kung’amua kwamba kweli ni Henry kutokana na wigi alilokuwa
amevaa, pia miwani ya macho ambayo iliwachanganya zaidi.
0 COMMENTS:
Post a Comment