Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Mbrazili, Andrey
Coutinho, amesema hatamani kuona kiungo wa timu hiyo, Mnyarwanda, Haruna
Niyonzima, anaihama timu.
Niyonzima anatarajia kumaliza mkataba wake
mwishoni mwa msimu huu na kuna taarifa kuwa amesharuhusiwa kuondoka.
Kauli hiyo, ameitoa Mbrazili huyo hivi
karibuni ikiwa ni siku chache tangu Niyonzima atangaze kuondoka mara baada ya
mkataba wake kumalizika mwishoni mwa msimu huu wa ligi.
Coutinho
alisema hakuna mchezaji anayemvutia akiwa ndani ya uwanja kama Niyonzima
kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuichezesha timu.
Coutinho alisema, kiungo huyo ana uwezo wa
kucheza soka nchi yoyote ikiwemo Brazil kutokana na kiwango chake huku akimtaka
kuongeza mkataba mwingine wa kuendelea kuichezea Yanga.
“Niyonzima
ni kiungo bora Yanga na hata kwenye ligi kuu, nimesema hivyo baada ya kuwaona
viungo wengi kwenye mechi mbalimbali nilizozicheza na kuziona katika ligi kuu.
“Ninakuhakikishia kuwa, Niyonzima ana uwezo wa
kucheza soka nchi yoyote ikiwemo Brazil, kwa maana ya kiwango cha soka, anacho
kikubwa, ni mchezaji ninayependa kucheza naye, hakika sitamani kumuona
anaondoka,” alisema Coutinho.
0 COMMENTS:
Post a Comment