March 27, 2015


HUU NDIO UJUMBE: unaweza kusema hivyo baada ya mshambuliaji wa Manchester United, Radamel Falcao kumpelekea ujumbe kocha wake Louis van Gaal kwa vitendo.


Falcao ambaye amekuwa akiwekwa benchi katika kikosi cha Man United, ametupia mabao mawili ndani ya dakika nne wakati timu yake ya taifa ya Colombia ikiivaa Bahrain katika mechi ya kirafiki.


Colombia iliyokuwa ugenini katika mechi hiyo ya kalenda ya Fifa, ilishinda kwa mabao 6-0 huku Falcao akifunga bao la tatu na la nne ndani ya dakika nne.

Licha ya kuwa kwao, Bahrain iliyo namba 103 kwa ubora wa Fifa, ilishindwa kufurukuta dhidi ya Colombia iliyoonekana kuwazidi kila kitu.


Kwa mabao hayo mawili, amefikisha mabao 55 na sasa Falcao ameshika nafasi ya pili kwa wachezaji waliofunga mabao mengi zaidi wakiwa na kikosi cha timu ya taifa ya Colombia.


WAFUNGAJI BORA COLOMBIA:
1 Arnoldo Iguaran 24 mabao, mechi 68
2 Radamel Falcao mabao 23 mechi 55
3 Faustino Asprilla mabao 20 mechi 57
4 Freddy Rincon mabao 17 mechi 84
5 VĂ­ctor Aristizabal mabao 15 mechi 66
6 Teofilo Gutierrez mabao 14 mechi 37
Adolfo Valencia mabao 14 mechi 37
8 Ivan Valenciano mabao 13 mechi 29
Antony de Avila mabao 13 mechi 54
10 James Rodriguez mabao 12 mechi 32

Willington Jose Ortiz mabao 12 mechi 49

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic