Mechi
hiyo kutokana na ukubwa wake imekuwa ikivuta watu wengi sana kuihudhuria na
kuifuatilia kupiria vyombo mbalimbali vya habari.
Wachezaji
wa Yanga na Simba walifanya moja ya jambo jema na la kihistoria kuhusiana na
vita dhidi ya mauaji ya ndugu zetu albino.
Suala hilo lilisimamiwa na mwandishi wa habari Henry Mdimu ambaye pia ni albino na Yanga na Simba wakakubali wazo lake.
Simba
na Yanga walivaa fulana wakionyesha kuguswa na wakipinga suala hilo, kwamba si sahihi
pia ni unyama wa kupindukia.
Jambo
jema, jambo la maana na wanapaswa kupongezwa kwa kuionyesha jamii wanapinga
upuuzi na imani potofu kama hizo.
Kupinga
kuwa eti viungo vya albino vina bahati na watu wanaweza kupata utajiri.
Ujinga
wa kiasi hicho umekithiri, Tanzania inaaibika mbele ya dunia kuwa ina watu
wanaoamini ushirikina hadi kushindwa hata kudhamini uhai wa binadamu wenzao.
Hilo ni
jambo jema kwa kuwa mashabiki wa Yanga au Simba wanaweza kubadili imani zao
kwamba kinachofanyika ni upuuzi mkubwa.
SALEHJEMBE
inaamini moja ya mambo muhimu yanayoihusu jamii ambayo Simba na Yanga wamewahi
kuyafanya ni kupinga mauji ya albino, hadharani.
Hongereni
Yanga na Simba kwa mlichokifanya, baada ya hilo, bado mna nafasi ya kuisaidia
jamii ya Watanzania kwa kuwa nayo inawaunga mkono.
0 COMMENTS:
Post a Comment