RUVU SHOOTING |
Uongozi
wa klabu ya Ruvu Shooting umetangaza kuwa kuanzia sasa watatumia mtindo wa “kupiga
bila ya kuangalia usoni”.
Msemaji
wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema mfumo huo unalenga kutaka kuirudisha Ruvu
Shooting kwenye reli baada ya kupoteza mechi iliyopita dhidi ya Ndanda FC ambao
walipoteza.
MASAU BWIRE... |
“Sasa
tutakuwa tukipiga bila ya kuangalia usoni, hii ndiyo staili yetu. Tutakuwa
tukiingia nayo uwanjani.
“Tunajua
mechi ijayo dhidi ya Polisi Moro ni ngumu lakini sasa ni kupiga bila ya
kuangalia ili tuwe safi.
“Ukianza
kuangalia watu usoni unaweza kujikuta unaingia kwenye huruma tu,” alisema
Masau.
0 COMMENTS:
Post a Comment