MASHITAKA.... |
Unaweza
kusema sasa kimenuka, Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji ameamua kumfungulia
mashitaka mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba, Musleh Al Rawah.
Taarifa
zinaeleza kwamba askari polisi wameanza kazi ya kumtafuta kiongozi huyo wa
Simba.
Manji
amefungua mashitaka akimtuhumu Musley kumsukuma mwanaye na kumjeruhi mara tu
baada ya mechi ya watani Yanga dhidi ya Simba ambao waliibuka na ushindi wa bao
1-0, jana.
RIPOTI YA DAKTARI INAYOONYESHA MTOTO WA MANJI ALIVYOUMIA... |
Habari
za uhakika huku SALEHJEMBE ikinasa vithibitisho vinavyoonyesha Manji kufungua
kesi hiyo kupitia mwanaye Mehbub Ally mwenye umri wa miaka 12 anayedaiwa
kusukumwa na Muslye kwenye lifti.
“Kweli,
Manji amefungua kesi ndugu yangu. Awali tuliona suala hili kama utani, lakini
inaonekana hataki mzaha kwa watoto wake.
“Tulimpeleka
mtoto wake kwenye hospitali mara tu baada ya tukio lile la kusukumwa pale
uwanja wa taifa na baadaye tukaenda hadi polisi na kufungua kesi.
“Unajua
Manji kakasirishwa sana na kitendo cha mwanaye kusukumwa, wakati tunaondoka
kurejea nyumbani, Ally alikuwa akilia kwamba mguu unauma ndiyo tukaenda
hospitali.
“Baada
ya kuonekana ameumia kidole cha mguu, kuna mfupa umeweka ufa, Manji
akachanganyikiwa, akawa mbogo,” kilieleza chanzo cha uhakika.
Jana,
Manji alitaka kumvamia Musley baada ya kudai alimsukuma mwanaye, lakini Musley
akasema ilikuwa bahati mbaya na aliahidi kumuomba radhi Manji na mwanaye kwamba
hakukusudia kufanya vile.
0 COMMENTS:
Post a Comment