March 26, 2015


Nahodha wa Chelsea, John Terry amesaini mkataba mpya na klabu yake ambao utamuwezesha kulamba pauni 150,000 kwa wiki.


Mkataba huo mpya wa Terry mwenye umri wa miaka 34 na Chelsea utamalizika mwishoni mwa msimu huu wa 2015-16.

Kocha Mkuu wa Chelsea, Jose Mourinho ameutaja mkataba huo kuwa ni sahihi na kusisitiza si asante kwa Terry, badala yake ni kutokana na uwezo anaopuonyesha.

Terry ameichezea Chelsea mechi 661 tokea mwaka 1998 alipocheza mechi yake ya kwanza kabla ya kupata namba ya uhakika katika kikosi cha kwanza mwaka 2000.


Beki huyo anaendelea kushikilia rekodi ya beki aliyefunga mabao mengi zaidi akiwa na Chelsea baada ya kupachika 64.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic