Timu ya
Taifa ya Malawi (The Flames) tayari imewasili leo jijini Mwanza majira ya saa
sita mchana, ikiwa na kikosi chake kamili kwa ajili ya mchezo dhidi ya Taifa
Stars siku ya Jumapili kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.
Malawi
imewasili ikiwa na kikosi chake kamili cha wachezaji 18 na kufikia katika hotel
ya JB Belimonte, wakiwemo wachezaji saba wanaocheza soka la kulipwa katika nchi
za Afrika Kusini, Congo DR, Msumbuji na Zimbabwe.
Wachezaji wa
kimataifa waliowasili ni nahodha Joseph Kamwendo (TP Mazembe -Congo DR),
Chimango Kayira (Costal de Soul - Msumbiji), Frank Banda (HBC Songo -
Msumbiji), Esau Kanyenda (Polokwane City - Afrika Kusini), Harry Nyirenda
(Black Leopards - Afrika Kusini), Limbikani Mzava (Celtic - Afrika Kusini)
Gerald Phiri (Caps United - Zimbambwe)
Wegine ni
McDonald Harawa (Hoyale FC), Richard Chipuwa (Wanderers), Lucky Malata
(Silver), John Lanjesi (Civo), Francis Mulimbika (Wanderers), John Banda (Blue
Eagle), Earnest Tambwe (Surestream) , Micium Mhone (Blue Eagle), Chikoti
Chiriwa (Red Lions), Peter Wadabwa (Silver) na Amos Khamula(Support Ballaton).
Mkuu wa
msafara ni Alexander Waya, Kocha mkuu Young Chimodzi, kocha msaidizi Jack
Chamangwana, kocha wa makipa Pillip Nyasulu, Daktari wa timu Levison Mwale,
Meneja wa timu Frank Ndawa na Afisa Habari James Sangala.
Kikosi cha
timu ya Taifa ya Malawi kinatarajiwa kufanya mazoezi leo saa 10 jioni katika
uwanja wa CCM Kirumba, huku siku ya jumamosi wakipata nafasi ya kufanya mazoezi
tena kwenye uwanja huo wa mchezo.
Kesho
jumamosi saa 5 kamili asubuhi kutafanyika mkutano na waandishi wa habari katika
hoteli ya La Kairo iliyopo Kirumba jijini Mwanza, kocha wa Stars Mart Nooij na
kocha wa The Flames Young Chimodzi wataongelea maandilizi ya mchezo wao wa Jumapili.
0 COMMENTS:
Post a Comment