TENGA |
Rais wa TFF, Jamal Malinzi
amesema Tanzania itampigia kura ya ushindi Rais Sepp Blatter wa Fifa.
Lakini Rais wa Cecafa,
Leodeger Tenga naye ameungana na Malinzi na kuamini huo ni msimamo sahihi.
Kwa maneno hayo, maana yake
Tanzania tayari imeweka wazi kuhusiana na msimamo wake wa kutompigia kura Luis
Figo ambaye ametangaza kupambana na Blatter.
Figo raia wa Ureno aliyeng’ara
katika soka akiwa na timu za Barcelo, Real Madrid na Inter Milan, hatapata kura
ya Tanzania.
Lakini kwa maneno ya Tenga,
inaonekana atakuwa na kazi ya kupata kura upande wa bara la Afrika.
Malinzi na Tenga wamesema
Blatter amekuwa na msaada mkubwa kwa Afrika kuhakikisha wanatimiza ndoto zao
kwa maendeleo ya soka.
Hata hivyo hakuweka wazi
nini hasa ambacho amekuwa akijitolea kuisaidia Tanzania au Afrika!
0 COMMENTS:
Post a Comment