Mechi namba 117
iliyowakutanisha Simba na Yanga katika uwanja wa Taifa, imeingiza jumla ya Sh milioni 436,756,000 kutokana na idadi ya watazamaji 49,758 waliokata tiketi
kushuhudia mchezo huo.
Watazamaji
309 walikata tiketi za VIP A, 1,310 VIP B, 1,533 VIP C, Rangi ya Machungwa
(Orange) 9,913 huku viti vya rangi ya bluu na kijani wakiingia watazamaji
36,693.
Mgawanyo wa
mapato ya mchezo huo ni VAT 18% sh.66,623.796, FDF timu mwenyeji sh.
17,415,300, FDF TFF sh.7,463,700, Gharama za tiketi sh.11,669,600.
Mgao wa
Uwanja sh. 50,037,540.51, Gharama za mchezo sh.28,354,606.29, Bodi ya Ligi
(TPLB) sh. 26,686,688.27, TFF sh.20,015,016.20, DRFA sh. 11,675,426.12, klabu
ya Simba sh. 115,086,343 huku Yanga wakipata sh.81,727.83.
Wakati huo
huo Ligi Kuu ya Vodacom itaendelea kesho siku ya jumanne katika uwanja wa
Jamhuri mjini Morogoro, wenyeji timu ya Polisi Morogoro watawakaribisha Ruvu
Shooting kutoka Mlandizi mkoani Pwani.
Siku ya
jumatano JKT Ruvu watawakaribisha Young Africans katika uwanja wa Taifa jijini
Dar es salaam, huku jijini Tanga Mgambo Shooting wakiwa wenyeji wa timu ya Azam
FC.
Aidha
mechi ya Kombe la Shirikisho (CC) barani Afrika kati ya Young Africans dhidi ya
timu ya FC Platinum ya Zimbabwe, itafanyika siku ya jumapili Machi 15, 2015
katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
0 COMMENTS:
Post a Comment