March 4, 2015


Licha ya kutokuwa na kasi kama msimu uliopita, klabu ya Mbeya City imefunguka kuwa matokeo wanayopata kwa sasa ni kawaida kwa sababu hakuna timu ambayo inaweza kushinda kila mchezo.


Timu hiyo msimu uliopita ilikuwa moto na kuweza kufanya vyema huku ikimaliza katika nafasi ya tatu na kuweza kuwafunika baadhi ya wakongwe kama Simba, Coastal Union na Kagera Sugar.

Mbeya City kwa sasa inashika nafasi ya 12 ikiwa na pointi 168 tu kwenye msimamo wa ligi.

Msemaji wa Mbeya City, Mohammed Kisanda maarufu kama Dismas Ten, alisema kikosi chao kipo vizuri lakini kwa sasa ni upepo tu unapita, mambo yatakuwa mazuri.

“Timu si kama inafanya vibaya sana, ni matokeo ya kawaida, hakuna timu ambayo kila siku inashinda kila mchezo, kuna sare, kufunga na kufungwa, watu walitambue hilo na wawe na subira.


“Tunapambana kuhakikisha tunarudi katika mstari kwa kushirikiana vyema na benchi la ufundi na bado hatujakata tamaa, tunajipanga na tutafanya vyema japo ligi ya msimu huu imekuwa na changamoto tofauti na ile iliyopita,” alisema Dismas.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic