Mrisho Ngassa atakuwa kati
ya wachezaji watakaoanza katika kikosi cha kwanza leo wakati Yanga ikiivaaa JKT
Ruvu.
Habari za uhakika kutoka
ndani ya Yanga zimeeleza kocha Hans van der Pluijm amempanga Ngassa baada ya
kuhakikishiwa na daktari, kwamba anaweza kucheza.
Jana, kulikuwa na hatihati
Ngassa angeweza kuikosa mechi hiyo na leo asubuhi alisema bado anajisikilizia.
Lakini taarifa hizo
zimesema Ngassa ataanza katika kikosi cha kwanza katika mchezo huo wa Ligi Kuu
Bara katika Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Kulikuwa na hofu, huenda Ngassa asianze mechi hiyo kutokana na kuwa majeruhi.
Lets hope for the best.
ReplyDeleteGod bless YANGA!