MSEMAJI WA DRFA, OMAR KATANGA (KUSHOTO)... |
Baada ya kumalizika kwa
michuano ya ligi ya mkoa wa Dar es salaam na timu za FFU na Zakhem kumaliza
katika nafasi ya kwanza kwenye makundi yao,kesho 20/03/2015 utapigwa mchezo
mmoja wa kusaka nafasi ya kuungana na mabingwa hao kushiriki michuano ya ligi
ya mikoa.
Mchezo huo wa mtoano
utakaopigwa katika uwanja wa Mizinga Kigamboni,utazikutanisha timu za Pan
Africa dhidi ya Changanyikeni ambazo zimemaliza katika nafasi ya pili kwenye
makundi yao.
Kwa mujibu wa kamati ya
mashindano ya chama cha kandanda mkoa wa Dar es salaam,DRFA,baada ya kumpata
mshindi katika mchezo huo, majina ya timu hizo tatu yatapelekwa shirikisho la
soka la Tanzania TFF.
Aidha, kamati hiyo chini
ya mwenyekiti wake Kenny Mwaisabula,imewashukuru mashabiki waliojitokeza kwa
wingi kwenye viwanja mbalimbali kushuhudua michuano ya ligi mkoa wa Dar es
salam tangu ilipoanza kutimua vumbi.
0 COMMENTS:
Post a Comment