Kumekuwa
na taarifa kiungo nyota, Raheem Sterling hatakubali kusainik mkataba mpya na
klabu yake ya Liverpool pamoja na kuwa imeongeza dau kubwa.
Liverpool
iko katika hatua za mwisho kutaka kumsainisha mkataba mpya ikiwa imeongeza
kitita cha pauni 180,000 ambacho atakuwa analipwa kwa wiki.
Lakini
taarifa kutoka kwa watu wa karibu wa Sterling zinaeleza hatasaini.
Hali
hiyo kidogo inaonekana kuwachanganya Liverpool, lakini uongozi wake umeendelea
kusisitiza una imani ataisaini.
Unachofanya
sasa uongozi huo wa Liverpool ni kuendelea kumsubiri hadi atakaporejea kutoka
majukumu ya timu ya taifa ya England ili kufanya naye mazungumzo.
0 COMMENTS:
Post a Comment