Pamoja na Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, jana kutofurika hadi pomoni, Simba na Yanga zimefanikiwa kuingiza zaidi ya Sh
milioni 430.
Habari za uhakika
ndani zimeeleza mechi hiyo iliyowakutanidha watani jana imeingiza kiasi hicho
kikubwa cha fedha kinachoonekana kuzidi kile cha mechi ya kwanza msimu huu
iliyoisha kwa sare ya 0-0.
“Zaidi ya Sh milioni
430, unajua Simba walijitahidi kuweka ulinzi wa kutosha kuepusha wizi. Mechi ya
mzunguko wa kwanza, watu walikuwa wengi zaidi lakini haikuingiza fedha nyingi.
“Nafikiri TFF
watatangaza kiasi hicho cha fedha leo na unaweza kupata uhakika ni mia nne na
thelathini na ngapi,” kilieleza chanzo.
Katika mechi ya jana,
Simba walifanikiwa kuwanyamazisha watani wao Yanga kwa kuwachapa bao 1-0.
0 COMMENTS:
Post a Comment