March 4, 2015


Kocha wa Simba, Goran Kopunovic amesema kikosi chake kinaendelea vizuri katika kambi yake ya Zanzibar.

Rais huyo wa Serbia amesema kwamba wachezaji wake wamekuwa wakifanya vizuri mazoezi, hali inayompa matumaini ya kufanya vizuri katika mechi ya Jumapili dhidi ya watani wao Yanga.

“Najua mechi inayokuja ni ya presha kubwa, lakini kikosi kinafanya vizuri, mazoezi yanendelea vizuri na hadi sasa ari iko juu.

“Bado tuna siku kiasi cha kuendelea na maandalizi na kila mmoja wetu anajua umuhimu wa mechi husika, hivyo wanajituma na mambo yanakwenda vizuri,” alisema Kopunovic.

Simba ilipiga mazoezi yake leo asubuhi na ilitarajia kuendelea na mazoezi hayo leo jioni.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic