Uongozi
wa Yanga umesema unatambua kwamba leoi Jumatano hakuna mechi yoyote ya Ligi Kuu
Bara ambayo wanastahili kucheza.
Kauli
hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Yanga, Dk Jonas Tiboroha ambaye amesema kikosi
chao kitaendelea na mazoezi kama kawaida mjini Bagamoyo.
Msemaji
wa Yanga, Jerry Muro jana alisisitiza kwamba watapaleka timu Uwanja wa Taifa
jijini Dar, leo kucheza dhidi ya JKT Ruvu.
“Tunajua
hakuna mechi, nielewe hivyo na programu ya mazoezi inaendelea kama kawaida,”
alisema Dk Tiboroha.
Alipoulizwa
kuhusiana na kauli ya jana iliyotolewa na msemaji wa klabu yake, akasisitiza.
“Tunajua
leo hakuna mechi, hadi Jumapili tutakapocheza dhidi ya Simba.”
Jana, Yanga walisisitiza wangepeleka timu uwanjani leo huku wakisisitiza kugomea mechi yao ya Machi 11 baada ya Bodi ya Ligi kuisogeza.
Yanga ilikuwa ikipinga kuahirishwa kwa mechi yao ya leo dhidi ya JKT na kusogezwa Machi 11, siku tatu kabla hawajashuka uwanja kuwavaa FC Platinum ya Zimbabwe katika Kombe la Shirikisho.
Viongozi wa Siasa wawe wa siasa na wa soccer wawe wa soccer. Jerry amekuwa maarufu sana kupitia tasnia ya siasa. Mpira ubaki kuwa mpira asikurupuke na kuanza kuongea kama suala lenyewe hajalifanyia uchunguzi.
ReplyDeletePia awe na mawasiliano ya karibu na katibu wake ili kuepuka kuwayumbisha watu.