Donald Ngoma wa FC Platinum (kushoto) akiwa katika harakati zake uwanjani.
Na Louis
Ngwako, Gaborone
Watanzania
wanaoishi mjini hapa, wametoa tahadhari kubwa kwa kikosi cha Yanga kabla ya
kuivaa FC Platinum ya Zimbabwe.
Mashabiki
hao wamemtaka Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van Der Pluijm kuwa makini na
mshambuliaji Donald Ngoma wa FC Platinum.
NGOMA (KUSHOTO) AKIPAMBANA UWANJANI... |
FC Platinum
itakutana na Yanga Machi 14, mwaka huu katika mechi inayofuata ya Kombe la
Shirikisho baada ya kuing’oa Sofapaka ya Kenya kwa kuifunga nyumbani na
ugenini.
Wakizungumza
jijini hapa, wameliambia Championi Jumatatu kuwa Ngoma amekuwa hatari sana kila
anapokutana na timu za Botswana.
“Tumeona
akicheza na timu za Botswana, jamaa ni hatari, anavaa jezi namba kumi na moja.
Ana kasi, anapiga mashuti sana.
“Hata mechi
mbili dhidi ya Sofapaka ya Kenya, zote amefunga. Lazima wamchunge, pia ni
mjanja sana hata kama yuko katikati ya mabeki wa timu pinzani,” alisema
Mtanzania aliyejitambulisha kwa jina moja la Humphrey huku akiungwa mkono na
wenzake.
Ngoma
amekuwa tegemeo katika safu ya ushambuliaji ya FC Platinum inayoonyesha kupania
kusonga mbele zaidi. Platinum iliifunga Sofapaka kwa mabao 2-1 katika kila
mechi na kusonga mbele kwa jumla ya mabao 4-2.
Yanga ndiyo
timu pekee ya Tanzania iliyofanikiwa kusonga mbele katika michuano ya
kimataifa, baada ya kufanikiwa BDF ya Botswana kwa jumla ya mabao 3-2.
Mabao mawili
ya straika Amissi Tambwe yaliibeba Yanga katika ushindi wa 2-0 Dar es Salaam,
wakati bao moja la Mrisho Ngassa kwenye kipigo cha juzi cha 2-1, ndilo
lililosaidia kuivusha timu hiyo katika hatua ya kwanza.
0 COMMENTS:
Post a Comment