Akiwa na miaka 12, tayari Steven Gerrard alikuwa
na ndoto ya kuwa nyota tegemeo wa kikosi cha Liverpool.
Maneno aliyasema alipohojiwa akiwa na miaka 12
katika stori iliyotoka katika gazeti mwaka 1992.
Sasa anaondoka mwishoni mwa msimu huu, miaka 22
baada ya kuitumikia Liverpool. Anakwenda kujiunga na LA Galaxy ya Marekani.
Kuondoka kwake hakuzuii yeye kuwa shujaa wa
Liverpool.
Ndoto zake akiwa na miaka 12 katika academy ya
Liverpool, zilikamilika kwa kuwa alinuia.
Hili ni somo kwa vijana miaka kumi au chini ya
hapo kwamba wanaweza kutimiza ndoto zao na hakuna haja ya kuwa waoga.
0 COMMENTS:
Post a Comment