Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm ametoa angalizo kwa wachezaji wake.
Pluijm raia wa Uholanzi, amewaambia wachezaji wake kuwa baada ya kuing'oa FC Platnum ya Zimbabwe na kufanikiwa kuingia katika raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho, lazima wajue wana jukumu la mechi za Ligi Kuu Bara.
"Wakati mwingine mnaweza kujisahau baada ya kukamilisha jukumu moja. Lakini muhimu ni jukumu linalofuatia na lengo letu ni kutwaa ubingwa wa Tanzania Bara.
"Nimezungumza na wachezaji na kuwaambia kwamba wanastahili kucheza wakijua kuna kitu ambacho kinasubiriwa kwa hamu na Wanayanga.
"Naamini wachezaji ni waelewa. Wanajua maisha yao ni kupambana kila wanapoingia kuitumikia Yanga lakini nimekuwa nikifanya hivyo kwa lengo la kukumbushana na kupata uhakika wa mambo," alisema Pluijm.
Yanga imefanikiwa kuing'oa FC Platnum kwa jumla ya mabao 5-2 na sasa itakutana na Etoile du Sahel ya Tunisia.
0 COMMENTS:
Post a Comment