Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Mecky Maxime
amesema ana imani kikosi chake kitainuka.
Maxime amesema wamekuwa wakipoteza mechi
mfululizo, hali inayowashangaza lakini wanaamini ndiyo matokeo ya mpira.
“Kila kitu chetu kipo vizuri, tunafanya
mazoezi vizuri na mambo yote yako vizuri. Lakini kinachotokea mbele yetu, kila
mmoja kinamshangaza.
“Ambacho tunaangalia mbele ni kuhakikisha
tunashinda na kupata pointi tatu muhimu,” alisema Maxime.
Mtibwa Sugar imebakiza mechi sita huku ikiwa
katika nafasi ya 14 katika msimamo wa Ligi Kuu Bara.
Mtibwa ilimaliza mzunguko wa kwanza wa ligi
hiyo ikiwa kileleni huku ikiwa imecheza mechi nane bila ya kupoteza moja.
0 COMMENTS:
Post a Comment